Kenya imeripoti maambukizi mapya 787 ya ugonjwa wa corona baada ya kupima 6,892 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Hii inafikisha 195,898 idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini huku kiwango cha maambukizi kikiwa 11.4%.

Idadi ya maafa imefikia 3,838 baada ya kufariki kwa wagonjwa 12 zaidi huku waliopona wakifikia 184,885 baada ya kupona kwa watu 424.

Wagonjwa waliolazwa hospitalini 1,259 huku wanaoshughulikiwa nyumbani wakiwa 3,758.