Baadhi ya walimu kutoka kaunti ya Marsabit wametishia kutorejea shuleni Jumatatu ijayo shule zikifunguliwa kutokana na hofu ya usalama wao.

Walimu hao wanasema wanaishi kwa hofu kutokana na mapigano ya kikabila ambayo yamekuwa yakishuhudiwa katika eneo hilo.

Walimu hao sasa wametoa makataa ya hadi kesho kwa vitengo vya usalama kuwahakikishia usalama wao la sivyo wataondoka eneo hilo na kushinikiza kuhamishwa hadi maeneo mengine salama.

Haya yanajiri siku moja baada tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa NCIC kufaulu kwenye mazungumzo ya kuleta amani ya kudumu na viongozi wa kaunti hiyo.