Mahakama ya Eldoret imekubali ombi la idara ya upelelezi (DCI) kumzuilia mshukiwa wa mauaji Evans Wanjala kwa siku 21 zaidi.

Mshukiwa mwenye umri wa miaka Ishirini kutoka Moi’s Bridge, Uasin Gishu anahusishwa na mauji ya watoto.

Hakimu wa mahakama hiyo Naomi Wanjiru ameruhusu kufufuliwa kwa mwili wa Grace Njeri anayedaiwa kuuawa na mshukiwa.

Njeri,21, alipotea Mei 21, 2020 kabla ya mwili wake uliokuwa umeoza kupatikana Juni 18, 2020 katika shamba la Soronoi.

Mahakama imeambiwa kwamba Njeri alizikwa bila baadhi ya sehemu zake za mwili.

Wanjala aliwapeleka wapelelezi wa DCI katika maeneo matano anakodaiwa kutekeleza mauaji.