Mahojiano ya kuwatafuta makamishna wanne wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini (IEBC) yatakamilika Ijumaa hii ya Julai 23.

Jopo linaloendesha mahojiano hayo chini ye uenyekiti wake Dr. Elizabeth Muli limewahoji wawaniaji watatu zaidi leo akiwemo Simeon Muket, Timothy Ole Naeku na Zippy Musyimi.

Muket ameliambia jopo hilo kwamba maeneo ambako watu hawajasoma yanafaa kuruhusiwa kuwa na wawaniaji ambao hawana vyeti vya digrii.

Muwaniaji wa pili Timothy Ole Naeku amekuwa na wakati mgumu kujibu maswali ya jopo hilo ikiwemo mchakato wa kuandaliwa kwa kura ya maoni.

Zippy Musyimi kutoka kaunti ya Embu amefunga ukurasa wa mahojiano hayo Alhamisi akiahidi kutumia uzoefu wake katika maswala ya usimamizi kuleta mabadiliko katika tume ya IEBC.