Naibu rais William Ruto na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga kwa mara nyingine wametofautiana kuhusu mchakato wa kubadilisha katiba.

Ruto akizungumza alipokutana na wafanyibiashara wadogo wadogo katika kaunti ya Machakos ameshikilia kwamba mjadala unaofaa kuendelea nchini wakati huu ni namna ya kuboresha maisha ya mwananchi wa kawaida.

Kwa upande mwingine, Odinga aliyekutana na makundi mbalimbali ya kidini mjini Mombasa amesisitiza kwamba marekebisho ya katiba yana umuhimu huku akimsuta Ruto kwa kupinga kubadilishwa kwa katiba kupitia kwa mchakato wa BBI.