Majaji wapya 27 wa mahakama ya Mazingira na ile ya Leba walioteuliwa rasmi hivi maajuzi wataripoti kazini Agosti 1 mwaka huu.
Jaji Mkuu Martha Koome amesema majaji wanane watafanya kazi siku nzima katika mahakama mpya ya Mazingira hatua ambayo imefikisha idadi ya majaji hao kuwa 34.
Mahakama hizo mpya zitakuwa Nyamira, Kilgoris, Siaya, Vihiga, Kwale, Isiolo, Homa Bay na Nanyuki.
Jaji Koome amesema hatua hiyo itachangia pakubwa katika kuharakisha mchakato wa kupatikana kwa haki.