Hospitali ya kitaifa ya Kenyatta imetoa notisi ya siku saba kuzika miili 418 iwapo wapendwa wao hawatajitokeza kuidai.

Katika notisi, hospitali hiyo inasema miili hiyo imekuwa katika hospitali hiyo kwa muda mrefu na hakuna aliyejitokeza kudai ni ya wapendwa wao.

KNH inasema baada ya kukamilika kwa siku saba, wataelekea watatafuta kibali cha mahakama kuzika miili hiyo ambayo majina yake yamechapishwa katika tovuti ya hospitali hiyo.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya kaunti ya Kisumu kuzika maiti 61 baada ya familia za waliofariki kukosa kujitokeza kuichukua kwa mazishi.