Kila familia iliyoathirika na mkasa wa kuanguka kwa trela la mafuta huko Siaya ambapo watu 15 walifariki itapewa msaada wa Sh50,000 amesema mbunge wa Gem Elisha Odhiambo.

Akiwahutubia wanahabari kufuatia mkasa huo, mbunge huyo ameirai wizara ya afya kuwapa waliojeruhiwa msaada zaidi ili kuwawezesha kupata matibabu.

Hata hivyo mbunge huyo amesema msaada huo hautoshi na kuwataka viongozi akiwemo rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati na kuwasaidia walioathirika.

Mkasa huo uliotokea Jumamosi usiku katika eneo la Malanga ulisababishwa na baadhi ya wakaazi kukimbilia kupora mafuta kufuatia ajali iliyohusisha lori la mafuta na lile la maziwa.