Kibarua cha kuwatafuta makamishna wanne wapya wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini (IEBC) limeendelea huku watu watatu zaidi wakihojiwa.

Mfanyikazi wa tume hiyo Naisiae Tobiko amefika mbele ya jopo hilo linaloongozwa na Dr. Elizabeth Muli ambapo ameonya dhidi ya kubadilishwa kwa sheria za uchaguzi miezi michache kabla ya uchaguzi.

Baadhi ya wawaniaji walitapatapa kujibu maswali huku Profesa Michael Lokuruka akikabiliwa na wakati mgumu kujibu maswali ikiwemo umuhimu wa karatasi za uchaguzi kuchapishwa nje ya nchi.

Profesa huyo pia amepigwa chenga na mchakato wa kuchagua maspika wa mabunge ya kaunti.

Masaibu sawia na hayo yalimkumbuka profesa Murshid Mohammed aliyefika mbele ya jopo hilo baada ya Lokuruka, mara si moja akikiri kutokuwa na ufahamu wa maswali aliyoulizwa.