Kaunti ya Kisumu imezika maiti 61 baada ya familia za waliofariki kushindwa kujitokeza.

Serikali ya kaunti ya Kisumu chini ya uongozi wake gavana Profesa Anyang Nyong’o imezika miili hiyo katika makaburi ya Mambo Leo baada ya kupata kibali cha mahakama.

Mkurugenzi wa afya katika kaunti hiyo Fred Oluoch amesema walitafuta ruhusa ya mahakama kuondoa miili hiyo ili kupata nafasi zaidi kwenye hifadhi za maiti.

Amesema miili 16 zaidi itazikwa kwenye kaburi la pamoja baada ya familia zao kukawia kuichukua.