Chama tawala cha Jubilee kinataka kuhesabiwa upya kwa kura za uchaguzi mdogo wa Kiambaa baada ya kushindwa kwa muwaniaji wake Kariri Njama.

Mkutano wa kamati kuu ya chama hicho uliohudhuriwa na naibu mwenyekiti David Murathe umeelezea kutoridhishwa kwao na matokeo ya uchaguzi huo ambapo Njuguna Wanjiku wa chama cha UDA alitangazwa mshindi.

Murathe amedai kuwa wana ushahidi wa kutosha kuonesha kwamba kura hizo ziliibiwa kwa faida ya muwaniaji wa UDA aliyepata kura 21,773 dhidi ya kura 21,263 alizopata Njama.

Kamati hiyo aidha imetangaza mipangilio ya kikifufua upya chama hicho baada ya kuoneshwa kivumbi kwenye chaguzi za hivi punde.