Kilichofanyika katika eneo bunge la Kiambaa na wadi ya Muguga ilikuwa ni mechi ya kirafiki baina ya chama cha Jubilee na United Democratic Alliance (UDA).

Haya ndiyo matamshi ya naibu rais William Ruto akizungumza Murang’a ambaye matokeo hayo yanaashiria kwamba siasa za taifa hili zimebadilika.

Nao wabunge wendani wa Ruto wameshabikia ushindi wa muwaniaji wa chama UDA Njuguna Wanjiku aliyeshinda uchaguzi mdogo wa ubunge Kiambaa.

Wakiongozwa na mbunge wa Kikuyu Kimani Ichungwa na mwenzake wa Kiharu Ndindi Nyoro wamesema ushindi huo unaashiria imani walio nayo wakaazi wa Mt. Kenya kwa siasa za Hustler.

Wanjiku amepata kura 21,773 dhidi ya kura 21,263 alizopata Kariri Njama wa chama cha Jubilee.

Huku Muguga

Chama cha Jubilee kiliibuka na ushindi katika baada ya kuhsinda UDA na kura 27 pekee.

Hii ni baada ya Joseph Mungara Githinji wa Jubilee kutangazwa mshindi kwa kupata kura 4,089 akifuatwa kwa karibu sana na Peter Thumbi Kamau wa UDA aliyepata kura 4,062.

Moses Gichau Mumbi wa Thirdway Aliance amepata kura 49 pekee huku Peter Njoroge akimaliza wa mwisho na kura 32.