Mwili wa afisa wa Polisi Caroline Kangogo umepelekwa katika hifadhi ya maiti ya Iten saa chache baada ya kuripotiwa kujiua kwa kujipiga risasi nyumbani kwa wazazi wake katika eneo la Anin kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Kamanda wa Polisi Elgeyo Marakwet Patrick Lumumba amesema marehemu ambaye amekuwa akitafutwa hakuzingumza na yeyote kabla ya kifo chake.

Kamishana wa Polisi eneo la Rift Valley George Natembeya amedai kuwa Kangogo alijipiga risasi mwendo wa saa moja leo asubuhi.

Natembeya anasema, Kangogo alifika nyumbani kwa wazazi wake na kuingia kwa bafu ya nje ambapo alijipiga risasi na kufariki papo hapo.

Mmoja wa ndugu zake amesema hawakuskia mlio wa risasi na badala yake walishtukia mwili wa mpendwa wao ukiwa kwa bafu.

Kangogo amekuwa akitafutwa kuhusiana na mauaji ya afisa mwenzake huko Nakuru John Ogweno na Peter Ndwiga huko Juja.