Wapiga kura katika eneo bunge la Kiambaa na wadi ya Muguga wanaelekea debeni kuwachagua viongozi wao huku madai ya kuwahoga wapiga yakiibuka.

Muwaniaji wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) Wanjiku Njuguna akiandamana na mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua wamedai kuwa wenzao wa Jubilee wanatumia maafisa wa serikali kuwahonga wapiga kura Kiambaa.

Hata hivyo mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC Wafula Chebuati amewaonya machifu dhidi ya kukaribia vituo vya kupigia kura.

Kwa upande mwingine, muwaniaji wa chama tawala cha Jubilee Kariri Njama akiandamana na viongozi akiwemo mbunge wa Kieni Kanini Kega wameelezea matumaini ya kushinda uchaguzi huo.

Awali,

Polisi walilazimika kuingilia kati kutuliza hali baada ya kundi la vijana kumtaka kiongozi wa waliowengi katika bunge la kitaifa Amos Kimunya kuondoka kutoka kituo cha kupigia kura cha Kimuga.

Vijana hao wanaogemea chama cha UDA wanadai kwamba Kimunya alikuwa anajaribu kushawishi wapiga kura kwenye uchaguzi huo.

Hata hivo Kimunya amejitetea dhidi ya madai hayo na badala yake kusema yeye ni ajenti wa chama cha Jubilee katika uchaguzi huo.

Kule Muguga

Muwaniaji wa chama cha PPK Peter Njoroge  ameelezea kuridhishwa kwake na jinsi zoezi hilo linaendele.