Makachero kutoka idara ya upepelezi (DCI) wamemshika Masten Milimu Wanjala,20, mshukiwa anayedaiwa kuhusika na utekaji nyara wa watoto wawili Shauri Moyo, Nairobi na kisha kuwaua.

DCI inasema mshukiwa amekubali kuwaua watoto hao Charles Bala,13 na Mutuku Musyoki, 12 waliopotea Juni 30 na July 7, 2021 mtawalio.

Wanjala anayeaminika kuwaua zaidi ya watoto 10 aliwaelekeza wapelelezi hadi eneo alipowaua watoto hao kisha kutupa miili yao huko Kabete.

Mshukiwa awali alikuwa amewasiliana na mamake Musyoki, Felista Wayua akiitisha kikombozi cha Sh50,000 ili kumuachilia mtoto huyo.

Mshukiwa huyo anaendelea kuhojiwa kubaini alikowatupa watoto wengine alioua kabla ya kufikishwa mahakamani.