Bei za mafuta zitasalia zilivyo kwa muda wa mwezi mmoja ujao imetangaza tume ya kudhibiti kawi nchini EPRA.

Lita moja ya Petroli itaendelea kuuzwa Sh127.14 jijini Nairobi, Mombasa Sh124.72, Nakuru Sh126.75, Eldoret Sh127.67 na Kisumu Sh101.17.

Wakaazi wa Nairobi watanunua mafuta taa kwa Sh97.85, Mombasa Sh95.46, Nakuru Sh97.76, Eldoret Sh98.68 na Kisumu Sh66.39.

Lita moja ya Diseli itaendelea kuuzwa Sh107.66 jijini Nairobi, Sh92.74 mjini Kisumu, Sh105.27 jijini Mombasa, Sh107.35 mjini Nakuru na Sh108.46 mjini Eldoret.