Mahojiano ya kuwatafuta makamishna wapya wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini (IEBC) yameendelea kwa siku ya tano leo huku baadhi ya waliokuwa wanahojiwa wakishindwa kujibu maswali.

Aliyekuwa kamishna wa tume ya uwiano na utangamo wa kitaifa (NCIC) Profesa Joseph Naituli alitapatapa kujibu baadhi ya maswali ikiwemo utaratibu unaofaa kufuatwa hadi kuandaliwa kwa kura ya maamuzi.

Naye aliyekuwa naibu mwenyekiti wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC Irene Keino amekabiliwa na wakati mgumu kuelezea mbona anafaa kuteuliwa kuwa kamishna wa IEBC licha ya kujiuzulu kutoka EACC.

Keino ametapatapa alipotakiwa kueleza jinsi alivyongatuka kutoka tume hiyo ilhali kulikuwa na pendekezo la kubuniwa kwa jopo kuchunguza mienendo yake.

Wakati uo huo…

Muwaniaji mwingine Irene Masit alijitetea vikali alivyotakiwa kutumia Kiswahili kujieleza na lakini mchakato wa kuwapa vijana vitambulisho kabla ya kuwapa kadi za uchaguzi ukampiga chenga.