Tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa nchini (NCIC) imekemea vikali mapigano ya kikabila yanayoshuhudiwa katika kaunti ya Marsabit.

NCIC kupitia kwa mwenyekiti wake kasisi Samwel Kobia imesema inasikitisha kuona kwamba mamia ya watu wameuawa huku maelfu ya wengine wakibaki bila makao kwenye vurugu hizo.

Kobia amemtaka Inspekta wa Polisi Hillary Mutyambai kuhakikisha kwamba wahusika wamechukuliwa hatua na zaidi kuzitaka asasi husika kuwapa msaada wa kibinadamu walioathirika.

Amewaonya viongozi kukoma kutoa matamshi ya chuki na kuwarai wakaazi wa Marsabit haswaa eneo bunge la Saku kukumbatia mazungumzo.