Wanaotaka kujaza nafasi za makamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC wamekuwa na wakati mgumu kujieleza kwa lugha ya Kiswahili.

Aliyekuwa naibu mwenyekiti wa chama cha mawakili nchini LSK Harriet Chiggai amelazimika kujibu maswali kwa Kiingereza baada ya kuwa vigumu kujibu maswali kwa lugha ya kitaifa.

Muwaniaji mwingi Florence Jaoko ambaye ni mwenyekiti wa zamani wa tume ya kitaifa ya kutetea haki za kibinadamu nchini (KNCHR) alijipata katika hali kama hiyo alipotakiwa kuelezea ni vipi atawasiliana na wapiga kura ambao hawajui Kiingereza.

Francis Wanderi aliyekuwa wa pili kwenye zamu Jumatatu ametetea utendakazi wake wakati akihudumu kama afisa mkuu wa IEBC katika kituo kimoja cha kupigia kura.

Jumla ya watu 36 walituma maombi kujaza nafasi nne za makamishna wa tume hiyo ya uchaguzi.