Ken Muyundo ameshtakiwa kwa jaribio la mauaji na kumjeruhi Phanice Chemutai akidhania kuwa ni afisa wa Polisi mtoro Caroline Kangogo katika soko la Kiminini.

Akifikishwa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Kitale Julius Ngarngar, Muyundo amekanusha mashtaka dhidi yake na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh200,000 pesa taslimu au mdhamini wa Sh500,000.

Muyundo kupitia kwa wakili wake Cliff Ombeta ameiambia mahakama kwamba yuko tayari kutumia mbinu zingine ikiwemo nje ya mahakama kutatua swala hilo.

Chemutai amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Kitale huku kesi hiyo ikitazamiwa kutajwa tena Julai 28, 2021.