Mwanamke mmoja kwa jina Phanice Chemutai anapokea matibabu katika hospitali ya Kitale baada ya kupigwa risasi na jamaa aliyedhani kwamba yeye ni askari sugu mwanamke anayetafutwa Caroline Jemutai Kangogo.

Ripoti ya Polisi inaonesha kuwa Ken Muyundo anayemiliki silaha alimpiga risasi Phanice kutoka kijiji cha Kaboiywo kimakosa baada yake kumpigia simu mara kadhaa akitaka kukutana naye.

Muyundo alimuwekea mtego na kukutana naye katika soko la Kaminini ambapo alimpiga risasi tumboni.

Madaktari wanasema mwanamke huyo anaendelea kupokea matibabu na yuko katika hali nzuri baada ya tukio hilo.

Kangogo anaendelea kuwachenga Polisi siku chache baada ya kudaiwa kuwaua kwa kuwapiga risasi wanaume wawili chini ya saa Ishirini na nne akiwemo afisa wa Polisi wa Nakuru John Ogweno.