Kikosi maalum cha kupambana na ghasia GSU kimetumwa Marsabit kufuatia mapigano ya kikabila ambayo yamesababisha maafa na uharibifu wa mali.

Inspekta Jenerali wa Polisi Hillary Mutyambai ameelezea kusikitishwa kwake na hali ya utovu wa usalama inayochochewa na wizi wa mifugo.

Ametoa wito kwa wenyeji kushirikiana na Polisi katika kurejesha amani huku akiwataka wahalifu wanaohusika na visa hivyo kujisalimisha.

Awali tulizungumza na mwanahabari wetu Peter Kasula kufuatia mapigano ya leo asubuhi yaliyotokana na kuuawa kwa watu wawili kwenye barabara ya Marsabit mjini kuelekea North Horr.