Rais Uhuru Kenyatta amekitakia kila la kheri kikosi cha Kenya kitakacholiwakilisha taifa kwenye mashindano yanayokuja ya Olimpiki mjini Tokyo Japan.
Akizungumza alipokipokeza kikosi hicho bendera kabla ya kuondoka nchini katika Ikulu Nairobi, rais amekisihi kuliwakilisha taifa vyema kwenye mashindano hayo yatakayoanza baadaye mwezi huu.
Wanariadha mahiri Hellen Obiri, Eunice Sum, Faith Chepngetich, Geoffrey Kamworor na Weldon Kipkurui wataongoza juhudi za kuwinda nishani katika mashindano hayo.