Mahakama ya Mombasa imehairisha kesi ya mauji dhidi ya mbunge wa Malindi Aisha Jumwa baada yake kudaiwa kuwaondoa mawakili wanne wanaomuwakilisha mshtakiwa mwenza Geofrey Okuto.

Jumwa na Okuto wameshtakiwa kwa mauaji ya mfuasi wa chama cha ODM Jola Ngumbao wakati wa kampeini za udiwani kwenye wadi ya Ganda mwaka 2019.

Mahakama imeambiwa kuwa mawakili Jared Magolo, Cliff Ombeta, Danstan Omari na Shadrack Wamboi hawataendelea kumuwakilisha Okuto kwenye kesi hiyo.

Okuto ameiomba mahakama kumpa muda zaidi kutafuta wakili mwingine kumuwakilisha.