Wakenya wanatahadharishwa dhidi ya kuhadaiwa na wakora kutoa pesa ili kupata kadi zao za Huduma Namba.

Tahadhari hii imetolewa na serikali kupitia kwa msemaji wake kanali mstaafu Cyrus Oguna ambaye amesema kadi hizo zinaendelea kutolewa bure kote nchini.

Akitoa hakikisho kwamba awamu ya pili ya usajili wa Huduma Namba utaanza hivi karibuni, Oguna amewasihi Wakenya wasipuuze ujumbe wa kuwataka kuchukua kadi zao kwenye simu zao.