Spika wa bunge la seneti Ken Lusaka amekubali kuwa ni yeye baba wa mtoto ambaye hajazaliwa kufuatia kesi iliyowasilishwa mahakamani na mwanamke mmoja.
Kupitia kwa wakili wake Peter Wanyama, Lusaka amesema yuko tayari kuwajibikia majukumu ya ulezi pindi mtoto huyo atakapozaliwa.
Hata hivyo Gavana huyo wa zamani wa Bungoma ameomba mahakama kumruhusu kutatua suala hilo nje ya mahakama.
Mwanamke huyo kupitia kwa wakili wake Danstan Omari amesema anataka kulipwa shilingi million 25 za kumlea mtoto huyo na pia kujengewa nyumba.
Hata hivyo Lusaka ameimabia mahakama kuwa anasubiri mtoto kuzaliwa kabla ya kuanza kujukumika, msimamo ambao mwanamke huyo amepinga.
Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 28 mwezi huu.