Rais Uhuru Kenyatta atatangaza tarehe mpya ya ziara yake kukagua maendeleo katika eneo la Ukambani siku moja baada ya kuhairishwa kutokana na kile kilitajwa kama kuhofia msambao wa corona.
Msemaji wa Ikulu Kanze Dena katika taarifa amesema uamuzi huu umeafikiwa baada ya rais kukutana na viongozi kutoka Ukambani wakiongozwa na kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka.
Kwenye ziara hiyo ambayo tarehe itatangazwa baadaye, rais Kenyatta ataandamana na viongozi wa eneo hilo huku taarifa hiyo ikiashiria kwamba masharti ya kuzuia msambao wa corona yatazingatiwa.
Viongozi wengine waliokuwepo kwa mkutano huo ni magavana Charity Ngilu (Kitui) na Alfred Mutua (Machakos), maseneta Mutula Kilonzo (Makueni), Enock Wambua (Kitui) na Agnes Kavindu (Machakos).