Kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa corona nchini kiko katika asilimia 9% huku visa vipya 185 vikidibitishwa katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Wizara ya afya inasema sampuli zilizopimwa katika muda huo ni 2,047 na kufikisha idadi ya visa hivyo kuwa 186,053.

Taifa vile vile limeandikisha idadi kubwa ya wagonjwa waliopona kwani walioruhusiwa kuondoka hospitalini ni 1,186 na kufikisha idadi hiyo kuwa 128,811.

Idadi ya maafa imeongezeka na kufikia 3,690 baada ya kufariki kwa wagonjwa 15 zaidi.

Takriban wagonjwa 1,151 wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini huku wengine 5,426 wakishughulikiwa nyumbani.