Rais Uhuru Kenyatta yuko mjini Lusaka, Zambia kuhudhuria ibada maalum ya mazishi ya mwanzilishi wa taifa hilo hayati Kenneth Kaunda.
Marais wengine ambao wako nchini humo kwa hafla hiyo ni Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe na Makqweetsi Masisi wa Botswana.
Marehemu Kaunda anatazamiwa kuzikwa Jumatano ijayo ambayo ni Julai 7.
Rais huyo wa kwanza wa Zambia huru maarufu kama KK aliaga dunia mwezi jana akiwa na umri wa miaka 97.
Mwaka 1950, Kaunda alikuwa mtu muhimu katika Vuguvu la kupigania uhuru wa Rhodesia ya kaskazini kutoka kwa Uingereza.
Alikuwa Rais wa kwanza wa Zambia mwaka 1964 na kuongoza taifa hilo kupitia miongo kadhaa ya utawala wa chama kimoja.
Alijiuzulu baada ya kupoteza katika uchaguzi wa vyama vingi 1991.