Washukiwa watano wamekamatwa wakijaribu kuchimba shimo wakiwa na makusudi ya kuingia kwenye benki ya Prime Bank tawi la OTC Ijumaa asubuhi.

Washukiwa hao; Charles Mugo, Fredrick Muderwa, Jesse Muriuki, Gabriel Mungai na Reuben Njuka walikamatwa na wapelelezi wa DCI wakijaribu kuingia kwenye benki hiyo iliyoko katika barabara ya Ukwala.

Genge hilo limepelekwa katika kituo cha Polisi cha Kamakunji.

Wapelelezi wa DCI walinasa vyuma vya kubomoa ukuta, misumeno na kamba kutoka kwa washukiwa.