Maambukizi mapya 376 ya ugonjwa wa corona yamedhibitishwa nchini baada ya kupima sampuli 3,831 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.
Idadi ya visa vya ugonjwa huo imeongezeka na kufikia 184,537 huku kiwango cha maambukizi kikiwa katika asilimia 9.8%.
Habari njema ni kwamba wagonjwa 910 wamepona katika muda huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 126,594, 6 zaidi wakifariki na kufikisha idadi hiyo kuwa 3,640.
Wagonjwa waliolazwa katika hospitali mbalimbali ni 1,127 huku wengine 5,722 wakishughulikiwa nyumbani.