Idadi kubwa ya Wakenya wangepiga kura kupinga marekebisho ya katiba kupitia BBI iwapo kura ya maamuzi ingeandaliwa leo umesema utafiti.

Utafiti uliofanywa na shirika la TIFA unaonesha kuwa asilimia 31% ya Wakenya wangepiga kura ya ‘LA’ ikilinganishwa na asilimia 19% ambao wangepiga kura ya ‘NDIO’.

Tom Wolf ni mtafiti wa shirika hilo.

Kwa mujibu wa utafiti huo ambapo watu 1,500 walihojiwa, asilimia 14% ya Wakenya bado hawajafanya maamuzi kuhusu iwapo watapinga au kuunga mkono mchakato huo.

Wakaopinga mchakato huo wametaja kuongeza nafasi za uongozi kama moja wapo ya sababu ya kupiga kura ya LA.

Asilimia 59% ya wafuasi wa ODM wangepiga kura ya NDIO ikilinganishwa na asilimia 25% ya wafuasi wa Jubilee.