Kuna matumaini kwamba kesi ya mauaji dhidi ya wakili Willie Kimani, mteja wake na dereva wa teksi kusikilizwa hadi mwisho.

Hii ni baada ya jaji Jessie Lessit ambaye amekuwa akisikiliza kesi hiyo kusema kuwa jaji mkuu Martha Koome amemuagiza kushughulikia kesi hiyo hadi mwisho kabla ya kupewa uhamisho.

Lessit alipandishwa ngazi hadi mahakama ya rufaa na kulikuwa na hofu kwamba huenda kesi hiyo ikaanza kusikilizwa upya.

Kesi hiyo saa itakuwa ikisikilizwa kila siku ya Alhamisi na Ijumaa kuanzia tarehe nane hadi tarehe 30 mwezi huu.

Kesi hiyo iekuwa ikisikilizwa kuanzia mwaka 2016.