Chama cha KANU kimetangaza kuwa kitamuunga mkono muwaniaji wa chama tawala wa cha Jubilee kwenye uchaguzi mdogo wa Kiambaa utakaoandaliwa Julai 15.

Mwenyekiti wa chama hicho Gideon Moi ametoa tangazo hilo la kumuunga Kariri Njama baada ya kukutana na wajumbe wa chama hicho kutoka Kiambu.

Na huku kampeini zikishika kasi, uchaguzi huo mdogo unatazamiwa kushuhudia ubabe wa kisiasa baina ya rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto ambaye anahusishwa na chama cha United Democratic Alliance (UDA) ambacho muwaniwaji wake ni Njuguna Wanjiku.