Bunge la kaunti ya Kisii kwa kauli moja limepitisha bajeti ya mwaka 2021-2022 inayogharimu Sh12.5b.

Bajeti hiyo imepitishwa baada ya kuwasilishwa bungeni na waziri wa fedha wa kaunti hiyo Moses Onderi.

Huduma za afya pamoja na ujenzi wa barabara vimepewa kipau mbele kwenye bajeti hiyo.

Madiwani wa bunge la kaunti hiyo wameungana kupitisha bajeti hiyo baada ya majuma kadhaa kuzozana kwenye vikao ambavyo zaidi ya mara moja vimeishia kukumbwa na vurugu.