Waziri wa Usalama wa ndani Dr Fred Matiang’i amesema serikali haitafunga mitandao ya kijamii kutokana na matamshi ya uchochezi wakati wa uchaguzi mkuu mwaka ujao.
Badala yake, Matiang’i amesema serikali itawachukulia hatua kali washukiwa ambao watakamatwa wakitumia mitandao ya kijamii kuzua hofu na kuchochea ghasia.
Akizungumza katika ukumbi wa mikutano wa Bomas wakati wa uzinduzi wa mikakati ya tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa NCIC, Matiang’i amewahakikishia wakenya usalama wao wakati na baada ya uchaguzi huo.
Kwa upande wake, naibu jaji mkuu Philomena Mwilu akizungumza katika hafla hiyo ameitaka NCIC kutafuta ushahidi wa kutosha kabla ya kuwafikisha washukiwa wa uchochezi mahakamani.