Patel Mansukh, mmiliki wa bwawa la Patel lililoua watu 48 amefariki.

Patel amefariki akipokea matibabu katika hospitali ya Aga Khan kutokana na matatizo ya moyo.

Chifu wa Solai Kiragu Maina anasema mfanyibiashara huyo alikimbizwa hospitalini wiki iliyopita kwa matibabu kabla ya kifo chake.

Bwawa hilo lililoko Solai kaunti ya Nakuru lilivunja kingo zake mwaka 2018 na kuua watu 48 na kuwaacha mamia ya wengine bila makao.

Mwanawe Perry Masukh ni miongoni mwa watu tisa walioshikwa na kushtakiwa kuhusiana na mauaji hayo lakini wakaachiliwa huru na mahakama kuu ya Naivasha kutokana na ukosefu wa ushahidi.