Mchakato wa kuwatafuta makamishna wapya wa tume ya huduma za walimu nchini (TSC) unatazamiwa kuanza rasmi baada ya kuapishwa kwa makamishna tisa wa jopo litakaloongoza shughuli hiyo.

Makamishna walioapishwa ni; mwenyekiti Thomas Koyier, Dr. Mary Gaturu; Charles Mutinda, Njoki Kahiga, Margaret Geno, Richard Kibagendi na Dr. Hellen Misenda.

Wengine ni naibu mwenyekiti Charity Kisotu, Eva Nyoike na Prof. Stanley Waudo.