Mashirika mbalimbali yasiyokuwa ya kiserikali yanasisitiza kwamba uchaguzi mkuu ujao ni sharti uandaliwe Agosti 9, 2022.

Katika taarifa, mashirika hayo ikiwemo KHRC na ELOG yameitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini (IEBC) kuhakikisha kwamba imejiandaa vilivyo kwa uchaguzi huo.

Miongoni mwa yale ambayo mashirika hayo yametaka yafanyike kuelekea kwa uchaguzi huo ni kutoa hamasisho kwa umma kuhusu zoezi la uchaguzi na usajili wa wapiga kura.