Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko amepigwa na mapigo mawili mahakamani baada yake kushindwa kubatilisha kuondolewa kwake na uteuzi wa Ann Kananu kama naibu gavana wa Nairobi.

Mahakama imezika hatima ya Sonko baada ya jopo la majaji watatu Said Chitembwe, Wilfridah Okwany na Weldon Korir kuamuru kwamba utaratibu uliotumika kumng’oa ikiwemo bunge la kaunti ya Nairobi hadi katika bunge la Senate ulifuata sheria.

Kwenye uamuzi mwingine,

Ann Kananu atasalia kuwa naibu gavana wa Nairobi baada ya mahakama kuu kukubaliana na uteuzi wake.

Jopo la majaji watatu Said Chitembwe, Wilfridah Okwany na Weldon Korir kwa kauli moja limeamuru kwamba uteuzi huo ulifuata sheria ikizingatiwa kwamba awali aliyekuwa gavana Mike Sonko alimteua Kananu kwa wadhifa huo.

Sonko aliwasilisha kesi mahakamani kupinga uteuzi huo kwa misingi kwamba haukufuata sheria.