Maafisa kadhaa wa jeshi KDF wamefariki baada ya helikopita yao ya angani kuanguka katika eneo la Ol Tepesi, Ngong, kaunti ya Kajiado mapema leo.

Bila kutoa idadi kamili ya maafisa waliofariki, msemaji wa KDF Zipporah Kioko amedhibitisha kuwa waliojeruhiwa wamekimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Familia za waliopoteza wapendwa wao kwenye mkasa huo zinajulishwa kuhusu maafa hayo huku uchunguzi ukianzishwa kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Idara ya jeshi inasema ndege hiyo ilikuwa kwenye shughuli za mafunzo kabla ya kuanguka mwendo wa saa mbili unusu leo asubuhi.

Picha kutoka eneo la mkasa zimeonyesha helikopta hiyo ikiteketea kiasi cha kutoonekana vyema.