Wizara ya fedha imetoa Sh43.5b zaidi kwa serikali za kaunti kulipa madeni wanayodaiwa na wafanyibiashara.
Waziri wa fedha balozi Ukur Yatani katika taarifa anasema deni hilo ni la hadi mwezi Aprili na atamalizia madeni ya mwezi Mei na Juni hivi karibuni.
Pesa hizo zinatolewa siku moja kabla ya magavana kutishia kufunga kaunti kwa sababu ya kukosa pesa kuendesha oparesheni zake ikiwemo kulipa mishahara.
Itakumbukwa kwamba serikali za kaunti zina muda wa hadi mwishoni mwa mwezi huu kulipa madeni ya wafanyibiashara.