Kampeini ya kutoa chanjo dhidi ya ugonjwa surua ama Measles kwa watoto walio na umri wa kati ya miezi tisa hadi miaka mitano itaanza rasmi Ijumaa hii ya Juni 25.

Katibu mwandamizi katika wizara ya Afya Dr. Mercy Mwangangi ametoa hakikisho kuwa chanjo hiyo ni salama na kuwataka wazazi au walezi kuwaleta wanao kuchanjwa.

Kaimu mkurugenzi wa huduma za matibabu katika wizara ya afya Dr. Patrick Amoth amesema chanjo hiyo inatolewa kufuatia mkurupuko wa ukambi nchini, na haswa katika kaunti za Mandera, Pokot Magharibi, Wajir, Garissa na Tana River.

Kaunti zingine ni; Baringo, Turkana, Elgeyo Marakwet, Busia, Homabay, Migori, Kisii, Kajiado, Nairobi, Bomet, Bungoma Kakamega, Narok na Vihiga.

Watoto Million 3.5 wanalengwa kwenye kampeni hiyo itakayokamilika Julai 5.