Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amekuwa kiongozi wa hivi punde kujitosa kwenye mjadala wa kuhairishwa kwa uchaguzi mkuu wa 2022.

Akizungumza kwenye kongamano la uchaguzi huru lililowaleta pamoja wadau mbalimbali, Kalonzo amesema mjadala huo haufai kuendelea hata kidogo kwa sababu katiba iko wazi kuhusu tarehe ya kuandaliwa kwa uchaguzi mkuu.

Kwa upnade wake, kiongozi wa chama cha NARC K Martha Karua ameitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC) kufungua sava za uchaguzi mkuu wa 2017 ili kuliwezesha taifa kurekebisha makosa yaliyotokea kabla ya uchaguzi wa 2022.