Mwakilishi wa wanawake wa kaunti ya Kiambu Gathoni Wa Muchomba amehama kambi ya rais Uhuru Kenyatta na kujiunga na kambi ya naibu rais William Ruto.
Wa Muchomba amekuwa miongoni mwa watetezi wakubwa wa rais Kenyatta katika eneo la Mlima Kenya na aliyepigia debe siasa za mrengo wa ‘Kieleweke’.
Ripoti za Wa Muchomba kujiunga na siasa za hasla zimedhibitishwa na picha zake na Ruto katika afisi zake zilizoko Karen.
Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro amesema wanasiasa zaidi kutoka eneo la Mlima Kenya watajiunga na kambi ya Ruto.