Vinara wakuu wa uliokuwa muungano wa upinzani NASA wanatazamiwa kutoa taarifa kuhusu hatima ya mrengo huo hivi karibuni.

Hii ni baada ya vigogo hao Musalia Mudavadi (ANC), Kalonzo Musyoka (Wiper) na Moses Wetangula (FORD K) kukutana Jumanne.

Chama cha ANC kupitia ukarasa wake wa Twitter kimesema Mudavadi, Kalonzo na Wetangula wameshauriana kuhusu maswala mbalimbali yenye umuhimu wa kitaifa.

Vigogo hao wamekutana huku wakimuandamana mwenzao wa ODM Raila Odinga kuwalipa deni la kisiasa baada ya kubainika kuna uwezekano wa kushirikiana na chama tawala cha Jubilee kinachoongozwa na rais Uhuru Kenyatta.