Kesi mbili ziinayopinga sharti la kuwataka wanaopania kuwania udiwani kuwa na digrii zinatazamiwa kutajwa tarehe saba mwezi ujao.
Mahakama imewaagiza walalamishi kuwapa wahusika kwenye kesi hiyo stakabadhi husika na wawasilishe majibu kwa muda wa siku 10 zijazo.
Mwanasheria mkuu, spika wa bunge la kitaifa na tume ya uchaguzi IEBC wametakiwa kuwasilisha majibu yao kabla ya kutajwa kwa kesi hiyo.
Kwenye kesi ya kwanza, mkenya Gloria Orwaba anadai kuwa kipengee hicho cha katiba kinaweka vizingiti visivyofaa kwa mtu ambaye anaruhusiwa kuwania viti hivyo chini ya kipengee cha 38 cha katiba.
Kwenye kesi ya pili, shirika la Sheria Mtaani na wakili Shadrack Wambui wanahoji kwamba janga la corona lilivuruga kalenda ya masomo mwaka jana na hivyo kuwatatiza waliokuwa wameenda shuleni kutafuta masomo zaidi kabla ya uchaguzi huo.