Kesi mbili zimewasilishwa mahakamani kupinga sharti la kuwataka wanaowania nafasi ya udiwani kwenye uchaguzi mkuu wa 2022 kuwa na digrii.

Kwenye kesi ya kwanza, mkenya Gloria Orwaba anadai kuwa kipengee hicho cha katiba kinaweka vizingiti visivyofaa kwa mtu ambaye anaruhusiwa kuwania viti hivyo chini ya kipengee cha 38 cha katiba.

Orwaba sasa anaitaka mahakama kuondoa kipengee hicho kwenye katiba kwa misingi kwamba kinawafungia nje wakenya wengi wanaotaka kugombea kuwa MCA lakini hawana digrii.

Kwenye kesi ya pili, shirika la Sheria Mtaani na wakili Shadrack Wambui wanahoji kwamba janga la corona lilivuruga kalenda ya masomo mwaka jana na hivyo kuwatatiza waliokuwa wameenda shuleni kutafuta masomo zaidi kabla ya uchaguzi huo.