Serikali imezindua kampeni ya wiki moja inayofahamika kama KOMESHA CORONA kuhamasisha umma kuzuia wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya corona.

Katibu wa kudumu katika wizara ya habari na mawasiliano Esther Koimett aliyezindua kampeni hiyo Nairobi amesema wanapania kuwakumbusha wananchi mbinu za kujikinga ikiwemo kudumusiha usafi, kuepuka kukaribiana na kuvalia barakoa.

Msemaji wa serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna aliyeandamana na Koimett amewahimiza wakenya kuzingatia masharti yaliyowekwa na wizara ya afya ili kuhakikisha kwamba taifa halijaingia katika wimbi la nne.

Oguna amewatahadharisha wakenya dhidi ya kukusanyika katika mikutano ya kisiasa akisema kwamba ni jukumu la kila mkenya kujikinga.