Idara ya upelelezi nchini (DCI) inawaomba waliobiwa na wakora katikati mwa jiji la Nairobi kuripoti ili kuwezesha kupatikana kwa haki.

DCI inasema imelazimika kuwaachilia huru washukiwa wa uhalifu walioshikwa katikati mwa jiji kwa sababu hakuna walalamishi wanaodai kuvamiwa na kuibiwa.

Idara hiyo vile vile inasema baadhi ya wale walipiga ripoti wanakosa kufuatilia kesi zao ili washukiwa kushtakiwa na hivyo kuishia kuwachiliwa kwa wahalifu hao.

Matukio ya watu kuvamiwa jijini Nairobi yamekuwa kero katika siku za hivi karibuni huku Inspekta wa Polisi Hillary Mutyambai akiahidi kwamba hatua makhususi zinachukuliwa kukabiliana na hali hiyo.